Home » Commercial » Boeing » Boeing 787 » MTANZANIA ALIYE SHIRIKI KUTENGENEZA NDEGE MPYA YA TANZANIA BOEING 787-8 DREAMLINER HISTORIA YAKE

VIDEO ZOTE ZA NDEGE MPYA YA TANZANIA BONYEZA HAPA …. https://www.youtube.com/playlist?list=PLT-mX0PCMUxfyc6Ur2yjqWcKMOEXTPcPi Ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner ni ya ukubwa wa wastani, yenye injini mbili inayotengenezwa na kampuni ya Boeing ya Marekani.
Matumizi yake ya mafuta ni wa asilimia 20 chini cha ndege ya ukubwa sawa na huo na ndiyo ndege ya Boeing inayotumia kiwango cha chini zaidi cha mafuta.
Injini zake zimejengwa kwa njia maalumu ili kupunguza sauti ndani na pia nje ya ndege kwa hadi asilimia 60.
Madirisha yake ni makubwa kuliko ya ndege zingine za ukubwa kama huo kwa asilimia 30. Wakati ndege mpya ya shirika la ndege la ACTL ya Boeing 787-8 ilipotua katika uwanja wa mwalimu Julius Nyerere siku ya Jumapili, ni wachache ambao wangedhania kwamba Mtanzania ni miongoni mwa wale walioitengeneza ndege hiyo.
Hatahivyo ukweli ni kwamba bwana George Jonas anayetoka katika mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa maafisa wa kiufundi aliyehusika katika utengenezaji wa ndege hiyo yenye viti 262, kwa jina Boeing 787-8 Dreamliner.
Injini za ndege hiyo zimejengwa kwa njia maalumu ili kupunguza sauti ndani na pia nje ya ndege kwa hadi asilimia 60 huku madirisha yake yakiwa makubwa kuliko yale ya ndege zingine za ukubwa kama huo kwa asilimia 30.
Jonas ambaye babaake alikuwa mwanajeshi wa Tanzania aliambia The Citizen nchini humo kwamba amekuwa akihusika katika uundaji wa ndege hiyo tangu 2015 akiwa mfanyikazi wa kampuni ya Boeing, kutoka Marekani ambayo huunda, kutengeza na kuuza ndege, roketi, Setlaiti na makombora.
Marekani imeshindwa kuwarejesha watoto wa wahamiaji kwa wazazi wao
Habari ya mwana huyo wa bi na bwana labani Mwanjisya inaanzia wakati alipokuwa mwanafunzi katika shule ya msingi ya Ubungo.
Ndege ya kmapuni ya BoeingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Hiyo ilikuwa kati ya mwaka 1985 na 1991, alisema akiongezea kwamba baada ya kukamilisha masomo yake ya shule ya msingi alijiunga na shule ya upili ya Azania mjini Dar es Salaam kwa masomo ya kawaida kabla ya kuelekea shule ya upili ya IIboru mjini Arusha kwa masomo tangulizi ya shule ya upili.
”Nikiwa IIboru, nilisomea sayansi na kushirikisha masomo ya Fizikia, Kemia na Hisabati”, alisema.
Alichaguliwa na kundi moja la raia wa Marekani waliokuwa wakitafuta kijana wa Tanzania aliyekuwa na maono ili kufanya kazi kwa miezi mitatu nchini Marekani.
”Nilijiona kuwa mwenye bahati. Sikujua mtu yeyote wakati huo na wazazi wangu hawakuwa na fedha za kunipeleka ng’ambo kusoma”, alisema bwana Jonas, akiongezea kuwa babake alikuwa akifanya kazi katika jeshi la Tanzania.
Pacha walioungana Tanzania wawasili Saudi Arabia kwa upasuaji
Masomo yake
Akiwa nchini Marekani, alituma maombi ya kutaka kusoma katika chuo kikuu na akafanikiwa kusajiliwa na chuo kikuu cha Wichita ambapo alisomea shahada ya uhandisi wa mitambo ya kielektroniki pamoja na hesabati.
Masomo hayo yalitarajiwa kumpeleka katika kampuni ya Bombardier, kampuni ya uchukuzi wa ndege ya Canada ilioko katika mji wa Montreal, Quebec.
Ndege ya shirika la ndege la Air Tanzania iliotengezwa na kampuni ya BoeingHaki miliki ya pichaIKULU TANZANIA
Alifanya mafunzo yake katika tawi la Bombaridier lililopo Wichita 2005, huku akihusika na utengezaji wa ndege za watu binafsi pamoja na zile za kijeshi.
Alifanya kazi katika kampuni hiyo kwa miaka minne kabla ya kujiunga na Boeing 2011 kama muhandisi wa kielektroniki wa mitambo ya ndege za kibiashara.
Alihusika na mifumo yote ya kuendesha ndege hiyo.
Wakati mmoja alipokuwa katika mtandao akapata tangazo la Boeing na kuamua kujaribu kutuma ombi.
”Siku moja nilipokuwa kazini nilipokea simu kutoka Boeing, ikinielezea kwamba nilikuwa miongoni mwa watu 50 walioorodheshwa katika mahojiano ya kazi. Walinitumia nauli ya ndege. Nilienda katika mahojiano hayo, nikiwa sina wasiwasi, kwasababu tayari nilikuwa nimeajiriwa na Bombadier”, alisema.#KUWA #MZALENDOBONYEZAALAMAYA #SUBSCRIBE HAPO CHINI KUPATA HABARI ZA NDEGE TANZANIA ………LIKE……..COMMENTS
KARIBU KWENYE CHANNEL YA AVIATION PEKEE TANZANIA COMMENT LIKE SUBSCRIBE

NAOMBA SURPORT YAKO KWA KU SUBSCRIBE NA COMMENTS TUU PLEA

Add comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Log In

Aircraft Sale

There are no ads matching your search criteria.

Categories